Rais Kenyatta Atia Saini Miswada Saba

RaisA� Uhuru Kenyatta leo katika ikulu ya Nairobi ametia saini miswada saba ukiwemo mswada wa mwaka 2016 kuhusu hongo uliopitishwa na bunge la kitaifa tarehe moja mwezi Disemba. Lengo kuu la sheria ya mwaka 2016 kuhusu hongo ni kupeleka vita dhidi ya ufisadi hadi katika sekta ya kibinafsi kwa kuharamisha ulaji hongo katika sekta hiyo. Aidha unawezesha ushikirishi mwafaka na mfumo wa uwajibikaji katika uzuiaji , uchunguzi na kushtakiwa kwa washukiwa wa ulaji na utoaji hongo. Mswada huo unatwikaA� jukumu la kisheria kila mtu atakayegundua kisa cha ulaji rushwa kuripoti kisa hicho kwa tume ya maadili na kupambana na ufisadi. Miswada mingine ni pamoja na mswada wa marekebisho wa mwaka 2016 kuhusu ulinzi wa mashahidi ,mswada wa marekebisho wa mwaka 2016 kuhusu mashindanoA� , mswada wa mwaka 2016 kuhusu uhalifu wa kudharahu mahakama, mswada wa mwaka 2015 kuhusu vyuo vikuu , mswada wa marekebisho wa mwaka 2016 kuhusu bima na mswada wa marekebisho wa mwaka 2015 kuhusu vikosi vya ulinzi vya Kenya.Naibu raisA� William Ruto alishuhudia kutiwa saini kwa miswada hiyo iliyowasilishwa kwa rais Kenyatta na spika wa bunge la kitaifaA� Justin Muturi na katibuA� Justin Bundi. Wengine waliokuwepo ni pamoja na kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa Aden Duale na wakili mkuu wa serikaliA� Njee Muturi.