Rais Kenyatta Atia Saini Kuwa Sheria Mswada Kuhusu Uthibiti Wa Kampuni Za Ulinzi Za Kibinafsi

Rais Uhuru Kenyatta leo asubuhi alitia saini kuwa sheria mswada kuhusu uthibiti wa kampuni za ulinzi za binafsi.Sheria hiyo mpya inaotoa mwongozo kuhusu jinsi A�kampuni za ulinzi za binafsi zitakavyoshirikianaA� A�na vikosi vya ulinzi vya kitaifa. Aidha sheria hiyo inapendekeza kusajiliwa kwa kampuni zote za ulinzi,kutolewa upya mafunzo kwa wafanyakazi wa kampuni hizo na kubuniwa kwa halmashauri ya kuthibiti shughuli za kampuni za ulinzi za binafsi. Halmashauri hiyo ambayo itakuwa na makao makuu yake jijini Nairobi,itaweka viwango na mfumo wa utendakazi kwa wafanyakazi katika sekta hiyo. Halmashauri hiyo itaongozwa na mwenyekiti atakayechaguliwa na rais.Rais Kenyatta pia ametia saini A�marekebisho ya sheria A�ya mwaka 2016 A�kuhusu vyama vya kisiasa .