Rais Kenyatta Ataka Ushirikiano Na Israel

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza viongozi wenzake katika muungano wa Afrika kuirejesha Israeli kuwa mtathmini katika shirika hilo la kanda. Rais anasema ipo haja kwa bara hili kusonga mbele na kutafuta upya ushirikianoA� na Israeli katika nyanja za usalama wa kanda na kilimo. Haya yanajiri huku waziri mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu, akifichua kwamba ziara yake barani Afrika inanuiwa kushirikiana na bara hili huku nchi yake ikinuia kurejesha uhusiano mzuri ambao ulizorota kati ya IsraeliA� na bara hili. Aliahidi kushirikiana na vikosi vya usalama vya nchi hii kwenye habari za kijasusi ambazo zitasaidia kuzuia mashambulizi ya kigaidi hapa nchini. Lakini nchi hii pia itanufaika pakubwa na ushirikiano na Israeli katika nyanja ya kilimo, Israeli ikiwa mshirika mkuu kwenye mradi wa kilimo cha unyunyiziaji mashamba maji wa Galana Kulalu.

Wanafunzi 45 kutoka taasisi mbali mbali jana waliagwa na marais hao wawili wanapoelekea nchini Israeli kujifunza teknolojia zinazohusiana na kilimo cha unyunyiziaji mashamba maji na kile cha kutumia mashini. Manufaa mengine ya ziara ya Netanyahu ni pamoja na ushirikiano katika sekta za afya na uhamiaji huku Israel ikitarajiwa kulegeza sheria zake za uhamiaji na kuondoa aina fulani za visa za usafiri ambazo zimeonekana kuwawekea Wakenya masharti magumu ya usafiri hadi nchini humo.