Rais Kenyatta Ashauriana Na Prince William Kuhusu Uhifadhi Wa Wanyama Pori

Rais A�Uhuru Kenyatta ameshauriana na Prince William wa Uingereza, ambaye alimtembelea katika Ikulu ya Nairobi.Rais Kenyatta na Prince William walijadiliana kuhusu nyanja ambapo nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana,ikiwemo uhifadhi wa wanyama pori. Rais Kenyatta alimshukuru Prince William kwa mchango wake katika uhifadhi wa wanyama pori,huku akiangazia hatua nchi hii imepiga katika kukabiliana na uwindaji haramu.Rais alimfahamisha Prince William kwamba mwezi ujao ataongoza hafla ya kuteketeza tani 120 za pembe za ndovu na tani 1.5 za pembe za vifaru,kuashiria kujitolea kwa nchi hii katika kupambana na biashara hiyo haramu,inayotishia urathi wetu. Kwa upande wake Prince William alimhakikishia rais kwamba ataunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kuwalinda wanyama pori. Prince William ambaye aliwasili hapa nchini leo asubuhi kwa ziara ya binafsi,ni rais wa shirika la United For Wildlife a�� linalojumuisha mashirika mengine saba maarufu duniani ya uhifadhi wa wanyama pori .A�