Rais Kenyatta arejea inchini baada ya ziara Marekania

Rais Uhuru Kenyatta alirejea nchini jana usiku baada ya kukutana na kufanya mazungumzo siku ya jumatatu na rais wa Marekani Donald Trump jijini Washington DC.Ndege iliombeba rais na ujumbe wake iliwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta muda mfupi kabla ya saa tatu usiku.

Alilakiwa na naibu wa rais William Ruto na mkuu wa jeshi la ulinzi la taifa Samsom Mwathethe,miongoni mwa maafisa wengine waandamizi wa serikali.

Maswala muhimu yaliopekechwa wakati viongozi hao wawili walipokutana katika ikulu ya White House ni pamoja na biashara,usalama na fursa ya uwekezaji.Rais Uhuru aliuelezea mkutano huo na Trump kuwa uliofanikiwa,huku akisema utaimarisha pakubwa uhusiano kati ya Kenya na Marekani.