Rais Kenyatta ampongeza mwenzake wa Uturuki kwa kuchaguliwa

Rais Uhuru Kenyatta amempongeza rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan na chama cha AK kwa ushindi wao kwenye uchaguzi wa urais. Katika ujumbe kwenye kitandazi cha tweet, rais Kenyatta alisema yeye binafsi na wakenya kwa jumla wanatarajia kuimarika zaidi kwa uhusiano baina ya nchi hizo mbili.  Mnamo Juni, mwaka- 2016, rais Erdogan alifanya ziara ya siku tatu hapa nchini akiandamana na kundi la wafanyibiashara-135 kutafuta mbinu za kukuza uhusiano wa kibiashara kati ya Kenya na Uturuki. Marais hao wawili walikubaliana kushirikiana katika nyanja za biashara na usalama huku Uturuki ikikubali kubadilishana habari za kijasusi na Kenya kwani nchi hizo mbili zimo kwenye kanda zilizoathiriwa na vitendo vya kigaidi.