Rais Kenyatta amkaribisha Isaac Ruto kwenye chama cha Jubilee

Rais Uhuru Kenyatta amemkaribisha aliyekuwa gavana wa kaunty ya Bomet Isaac Ruto kwenye chama cha Jubilee ili aweze kufanya kazi na serikali kwa manufaa ya nchi hii. Akiongea wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa kavana mteule wa kaunty ya Bomet Dakt. Joyce Laboso, rais alimpongeza Ruto kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kukubali kushindwa na kukabidhi mamlaka.A�Rais pia alisema kwa jubilee kuwa na magavana wengi, maseneta, wabunge na wawakilishi wa wadi, ni thihirisho tosha kwamba wakenya walikipigia chama hicho kura kwa wingi ili kiweze kuendeleza nchi hii. Rais Kenyatta alisema ingawa upinzani una haki ya kwenda mahakamani, lingekuwa jambo la busara kwao kukubali kushindwa na kuwawezesha wakenya kuendelea na ajenda yao ya maendeleo. A�Rais Kenyatta wakati huo huo amewapongeza wakenya kwa kuwapigia kura wanawake wengi ili kuwawezesha kuchukua nyadhifa za uongozi akisema hii inaonyesha ukomavu wa demokrasia.