Rais Kenyatta akutana na waakilishi wa kenya katika bunge la EALA

Rais Uhuru Kenyatta jana alikutana na wawakilishi wa Kenya katika bunge la Afrika mashariki (EALA) na akawahimiza kuendeleza maslahi ya nchi hii wanapojadili hatua za kuharakisha muungano wa eneo hili. Rais aliwaambia wabunge hao wa EALA kutilia mkazo umoja utakaohakikisha ufanisi wao katika kuimarisha maslahi ya nchi hii katika bunge hilo la Afrika Mashariki. Akiongea katika Ikulu ya Nairobi, Rais aliwataka wabunge hao kuhakikisha kuwa tofuati za kisiasa za hapa nchini hazitatizi utendakazi wao wanapohudumu katika bunge hilo lililoko Tanzania. Aliwahakikishia wabunge hao kwamba atashirikiana nao kwa karibu na kuanda mikutano ya mara kwa mara kuhakikisha kuwa ziara yao ya kikazi katika bunge hilo inaleta manufaa kwa wakenya na eneo la Afrika mashariki kwa ujumla. Wabunge hao ni pamoja na Simon Mbugua, Kennedy Kalonzo, Kennedy Kalonzo, Wanjiku Muhia, Nooru Adan, Florence Jematiah, Mpuru Apuri na Abdikadir Omar Aden