Rais Kenyatta ajivunia mtaala mpya

RaisA�A�Uhuru Kenyatta amewahakikishia wazazi kuwa mageuzi ya mtaala katika sekta ya elimu yanaendelea akisema mageuzi hayo yatakuwa moja ya urathi mkubwa wa serikali yake. Wakati huo huo rais ameagiza wizara ya usalama wa kitaifa kuhakikisha makamishna wa kimaeneo wanashirikiana na washirikishi wa kimaeneo wa elimu ili kuandaa makongamano ya wadau katika maeneo yote ya nchi ili kuelimisha umma na pia kusikia maoni ya wananchi kuhusu mtaala huo mpya. Akiongea leo wakati wa uzinduzi wa msafara wa magari unaosafirisha vitabu vya mtaala mpya kote nchini katika mtaa wa Karen jijini Nairobi, rais Kenyatta aliongeza kuwa hakuna sababu ya shule za kibinafsi na zile zilizojengwa kwa msingi wa kidini kununua vitabu kwa bei ghali. RaisA�A�Kenyatta alisema ipo haja ya kusawazisha watoto wote hapa nchini kwa kuwapa rasilimali zinazohitajika ili waweze kujiimarisha.

Serikali hivi majuzi ilibuni sera mpya ya usambazaji wa vitabu ambayo inazuia mawakala na kuwawezesha wachapishaji kusambaza vitabu akida moja kwa moja katika shule.