Rais kenyatta Aisihi UNCTAD Kuzingatia Mabadiliko Yatakayo Leta Ufanisi.

Rais Uhuru KenyattaA� ametoa wito kwa viongozi wa kimataifa wanaohudhuria kongamano la umoja wa mataifa kuhusu biashara na maendeleo, kuzingatia mabadiliko ambayo yataleta ufanisi.Rais Kenyatta amesema mkutano huo wa juma moja unatoa fursa kwa mataifa kubadilishana maoni kuhusu jinsi maamuzi yanavyoweza kutekelezwa.Akiongea wakati wa ufunguzi rasmi wa kikao cha nne cha mkutano wa UNCTAD, rais Kenyatta alitoa wito wa kutolewa kwa mapendekezo mapya kuhusu jinsi ya kustawisha uchumi wa mataifa ya kiafrika.Akiongea wakati wa hafla hiyo ,katibu mkuu wa umoja wa mataifa l Ban Ki-Moon aliwahimiza viongozi waliohudhuria mkutano huo kuhaikisha kuna usawa wa kiuchumi duniani.Ban Ki Moon aliongeza kwamba changamto za kiuchumi duniani zinahitaji sera mpya kuimarisha biashara. Ban Ki Moon alitoa wito kwa mataifa yanayohudhuria kongamano hilo kubunge sera zinazohimiza usawa.Katibu mkuu wa kongamano hilo la UNCTAD Dr Mukhisa Kituyi alisema wakati umewasili kwa viongozi wa kimataifa kuangazia mbinu za kuimarisha maendeleo.