Rais Kenyatta ahimiza wakazi wa Kilifi kumpigia kura

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wakazi wa kaunti ya Kilifi kumpigia yeye kura pamoja na wagombezi wengine wa chama cha Jubilee, akisema upinzani hauna ajenda ya maendeleo kwa nchi hii. Akiongea jana alipofanya kampeni huko Malindi, Rais aliwaambia wakazi kutopigia kura upinzani akisema nia yao ni kujitakia makuu na wala sio maslahi ya mwananchi wa kawaida. Alisema kuwa ajenda ya Jubilee ni kuwahudumia Wakenya wote million 45 bila kujali miegemeo yao kisiasa. Rais alikuwa ameandamana na naibu wake William Ruto aliyedai kuwa upinzani umehisi kushindwa na sasa unataka kutumia mahakama kuchelewesha uchaguzi. Rais aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kwamba serikari yake itasugulikia swala la maskwota jinsi imefanya maeneo mengine ya pwani.