Rais Kenyatta ahimiza wafuasi wake kujitokeza kwa wingi kumpigia kura

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wafuasi wake wajitokeze kwa wingi hapo agosti 8 ili kumpigia kura yeye na wagombea wengine wa chama cha Jubilee. Rais alitoa wito huo aliporejea katika kaunti za Nyeri na Muranga��a kukipigia debe chama cha Jubilee.A� Alisema mafanikio ya serikali yake katika muda wa miaka minne iliyopita ni ya kufana na yalitokana na hali ya maelewano yaliyokuwepo katika utawala wake. Rais anafanya kampeini akielezea mpango wake wa kuwasilisha ufanisi kwa wakenya wote ukiwemo utoaji ajira zaidi, kupunguza gharama ya maisha na kudumisha amani na usalama kwa Wakenya wote. Kiongozi wa taifa ambaye aliwahutubia wafuasi huko Mukuruweini katika eneo-bunge la Mukurweini na Kiandu katika eneo-bunge la Tetu, alitoa wito kwa wakazi kuendelea kudumisha amani. Rais amepangiwa kuhutubia mikutano zaidi katika kaunti ya Nyeri kabla ya kuelekea kaunti ya Muranga��a kwa ziara nyingine ya kukutana na wananchi. Katika muda wa wiki mbili zijazo Rais anatarajiwa kuzuru angalau kaunti 30, ambapo itakuwa ni mara ya pili kuzuru baadhi ya kaunti hizo.