Rais Kenyatta Ahimiza Ushirikiano Wa Kibiashara Kati Ya Ufaransa Na Kenya

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza waagizaji bidhaa wa Ufaransa kushirikiana kwa karibu na wauzaji bidhaa wa humu nchini ili kuimarisha uuzaji bidhaa za humu nchini , nchini Ufaransa na mataifa mengine ya ulaya. Rais alisema hatua hiyo itaondoa vizingiti ambavyo vimezuia bidhaa za humu nchini hasa zile za kilimo kufika katika soko la Ufaransa, akiongeza kusema kwamba hatua hiyo pia itasaidia kuziba pengo la kutokuwaA� kwaA� usawa wa kibiashara ambalo kwa sasa linanufaisha zaidi Ufaransa. Akiongea jana mjini Paris, Ufaransa, wakati wa mkutano na waagizaji bidhaa wa Ufaransa ambao waliongozwa na mwenyekiti A�Perre Layani wa soko la kimataifa la Rungis, ambalo ndilo soko kubwa zaidi duniani la uuzaji kijumla bidhaa za A�mazao mabichi, kiongozi wa taifa aliwahimiza wawekezaji wa Ufaransa kushirikiana na wenzao hapa nchini katika kuongeza thamana ya bidhaa za kilimo kutoka hapa nchini ili kuwezesha kutayarishwa bidhaa bora ambazo zitatimiza viwango vya kimatifa. Rais Kenyatta alisema kuongezeka kwa bidhaa za Kenya katika soko la Ufaransa pia kutasaidia kubuni nafasi za ajira kwa vijana wa humu nchini. Kwa upande wake Layani alimhakikishia rais Kenyatta kwamba shirika lake liko tayari kushirikiana na wauzaji bidhaa wa humu nchini ili kuafikia uuzaji bidhaa zaidi za humu nchini katika soko la Ufaransa.