Rais Kenyatta aendeleza kampeini zake kabla ya marudio ya uchaguzi wa urais

Rais Uhuru Kenyatta kwa wakati huu anazuru kaunty ya Pokot Magharibi kisha kuzuru kaunty za Bungoma na Uasin Gishu huku akiendeleza kampeini zake kabla ya marudio ya uchaguzi wa Urais tarehe 17 mwezi ujao.Kulingana na hatibu wa Ikulu, Rais atatumia ziara hiyo kuwashukuru wakazi kwa kudumisha amani na kuwapigia kura viongozi wa Jubilee A�kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe 8 mwezi agosti. Katika kaunty ya Bungoma Rais Kenyatta atazuru eneo bunge la Kimilili hususan kuwashukuru wakazi wa eneo bunge hilo kwa kumpigia kura mbunge wa jubilee Didmus Wekesa Baraza. Hapo kesho rais atapeleka kampeini zake katika kaunty za Kericho na Nakuru A�ambapo atawahutubia wakazi huko A�Kapkatet na Naivasha.