Rais Kenyatta adumisha uongozi wa mapema

Mgombea urais wa chama cha Jubilee, Uhuru Kenyatta, anaongoza katika uchaguzi wa urais kwa kura 7,092,508 zilizohesabiwa kulingana na matokeo yaliyotolewa na tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC). Raila Odinga wa muungano wa (NASA) yuko katika nafasi ya pili kwa kura 5,721 889. Joseph Nyaga yuko nafasi ya tatu kwa kura 31 656 na anafuatiwa na Mohamed Abduba Dida kwa kura 26,795. Ekuru Aukot wa chama cha Third Alliance amepata kura 22 561, Japheth Kavinga Kaluyu ana kura 9 616 akifuatiwa na Cyrus Jirongo kwa kura 9,299 naye Michael Mwaura, ambaye ni mgombea huru amepata kura 7,422.
Matokeo hayo yanatoka kwenye jumla ya vituo 34,713 vya kupigia kura kati ya vituo 40,883. 331,846 zimekataliwa.