Rais Kenyatta achukua uongozi wa mapema

Rais Uhuru Kenyatta amechukuwa uongozi wa mapema katika marudio ya uchaguzi wa tarehe 26 mwezi Oktoba huku matokeo yakiendelea kumiminika kutoka vituo mbali mbali vya uchaguzi kote nchini . Rais Kenyatta anaongoza kwa wingi wa kura akifwatiwa kwa karibu na mpinzani wake wa karibu Raila Odinga ambaye alijiondoa katika kinyanga��anyiro hicho na kusema ni uchaguzi usio huru na haki.

Wakenya walipiga kura hapo jana kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu uliofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 8 Agosti kwa misingi kuwa tume ya IEBC ilitekeleza kasoro nyingi za uchaguzi wakati wa uchaguzi . Katika uamuzi huo wa tarehe 1 mwezi Septemba , mahakama iliagiza uchaguzi wa urais kurejelewa baada ya siku 60 kulingana na katiba. Odinga aliwahimiza wafuasi A�wake kutoshiriki katika kura hiyo hata baada ya rais A�Uhuru kuwahimiza watu kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Tume ya A�IEBC ina siku saba kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo huku mjadala ukiendelea kuhusiana na uhalali wa kura hiyo.