Rais Kenyatta Aahidi Uchaguzi Ujao Utakuwa Huru Na Wa Haki

 

Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kwamba uchaguzi mkuu ujao utakuwa huru na wa haki. Akiwahutubia wakenya jijini Berlin Ujerumani hapo jana usiku, Kenyatta alisema kuwa mashauriano yanaendelea kati ya tume huru ya uchaguzi na mipaka na wizara ya fedha kuhusu kutafuta pesa za kufadhili uchaguzi huo mkuu. Alisema kuwa serikali itatafuta pesa za kufadhili usajili wa wakenya wanaoweza kujiandikisha kama wapiga kura hapa nchini na pia ughaibuni na kuongeza kuwa wakenya walioko nga��ambo wana haki sawa ya kujisajili kama wapiga kura na kushiriki katika kuwachagua viongozi wao wa siku za usoni.Rais pia aliwahimiza wakenya walioko nga��ambo kuwekeza katika miradi mbali mbali iliyoko ikiwa ni pamoja na miundo msingi pamoja na kawi inayoweza kurejelewa matumizi inayotumika zaidi ujerumani . kundi hilo la wakenya pia lilihutubiwa na mkewe rais Margaret Kenyatta, aliyeahidi kufanya kazi ili kuimarisha sekta ya afya hasa katika kuhakikisha kuwa akina mama hawafariki wanapojifungua watoto.