Rais Jacob Zuma ajiuzulu

Rais Jacob A�Zuma A�wa Afrika kusini, A�amejiuzulu ili kuepuka kura ya kuto-kuwa na imani naye bungeni ingawaje angali hakubaliani na uamuzi wa chama cha ANC wa kumshinikiza ajiuzulu. Kujiuzulu kwa Zuma kunamaanisha naibu rais Cyril Ramaphosa ndiye kaimu rais lakini sharti aapishwe kwa utiifu na uaminifu kwa jamhuri na katiba anapotwaa majukumu na urais. Zuma ndiye rais wa pili wa chama cha ANC kujiuzulu kama kiongozi wa nchi hiyo baada ya aliyekuwa rais Thabo Mbeki kujiuzulu mwaka wa 2008. Zuma alitimiza muda wa makataa wa saa 48 katika jengo la serikali la Union Buildings mjini Pretoria jana usiku. Alianza kutoa hotuba yake kwa mzaha na wanahabari, ambao walikuwa wamepiga kambi nje ya jengo la Union Buildings. Zuma alizingatia maadili ya kidiplomasia kwenye hotuba yake na hakuonekana kuwa na ghadhabu kama ilivyojiri hapo awali kwenye mahojiano na shirika la utangazaji nchini Afrika SABC siku moja kabla ya kujiuzulu kwake.