Rais Hassan Mahammud Wa Somalia Ahimiza Wakimbizi Kambini Dadaab Kuheshimu Agizo La Kenya Kurejea Nchini Mwao

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amehimiza wakimbizi wanaoishi kwenye kambi ya Daadab kuheshimu agizo la Kenya la kurejea nchini mwao. Rais Hassan Sheikh Mohamud alitoa tangazo hilo baada ya kushauriana na rais Uhuru Kenyatta huku akiahidi kwamba A�zoezi hilo litatekelezwa kwa njia bora inayotilia maanani maadili ya utu. Rais huyo aliye ziara humu nchini pia alielezea shukrani zake kwa serikali na watu wa Kenya kwa kuwapatia makaazi raia hao wa Somalia kwa muda wa miaka 25 sasa. Rais Muhamud aliwahakikishia watu wake klwamba serikali yake iko tayari kuwapokea ili washiriki katika juhudi za kuijenga upya nchi yao, na pia taratibu za matridghiano. Pia aliwahakikishia kwamba taratibu za kuwarejesha makwao, zitakuwa za kibinadamu kuambatana na makubaliano ya pande tatu. A�Rais Muhamud alitoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa usaidizi wa kutosha kwa serikali yake inapowapokea wakimbizi hao.