Rais Barack Obama amesifu ufanisi ulioafikiwa katika vita dhidi ya kundi la Islamic State

obama

Rais Barack Obama wa marekani amesifu ufanisi ulioafikiwa katika vita dhidi ya kundi la Islamic State lakini akaonya kwamba kundi hilo bado linaweza kuchochea na kutekeleza mashambulizi makali.

Akiongea baada ya kukutana na maafisa wakuu katika makao makuu ya polisi yaA�Pentagon, Obama alisema kuwa kundi hilo litaendelea kuwa tishio huku akizungumzia uwezo wa kundi hilo wa kuwachochea wafuasi wake kutekeleza mashambulizi madogo ambayo hayawezi kugunduliwa na kuzuiwa kwa urahisi.
Kundi hilo limedai kuhusika kwenye mashambulizi kadhaa ambapo watu wengi wameuawa likiwemo lile la kutumia lori jijini Nice nchini ufaransa mwezi uliopita ambapo watuA�84 waliuawa na pia kisa cha ufyatuaji risasi jijini Orlando, Florida, ambapo watu 49 waliuawa.
Obama alisema ni sharti marekani iimarishe juhudi za kukabiliana na kundi hilo na kunasa jumbe kwenye mitandao ambazo huenda zikawafikia watu na kuwafanya kutekeleza maovu. Alisema kukomeshwa kwa uhasama nchiniA�
Syria sharti kujumuishe kukomeshwa kwa mashambulizi ya angani na mbinu nyingine zinazotumiwa na serikali ya Syria kuwaua raia.