Rais Barack Obama Akashifu Mauaji Ya Louisiana

Rais wa Marekani Barack Obama amesema mauaji ya kinyama ya raia wawili weusi wa Marekani yaliyofanywa na polisi ni miongoni mwa visa vinavyotokea mara kwa mara katika taifa hilo naA� kwamba yanapaswaA� kuwatia hamasa wamarekani kuungana, ili kukabiliana na tatizo hilo.Maandamano yamekuwa yakiendelea tangu kulipotokea mauaji hayo siku ya jumatano kwenye kizuizi cha ukaguzi wa magari A�cha polisi A�jimboni Minnesota.Maandamano hayo yalianza kufwatia mauaji ya Philando Castile na polisi huko Louisiana.Kisa hicho kinafwatia msururu wa visa vya aina hiyo vya wamarekani weusi vilivyozuia taharuki na chuki na kuibua mjadala wa kitaifa kuhusu utumizi wa nguvu kupita kiasi na maafisa wa polisi.Kwenye taarifa,rais Obama alisema kisa hicho ni dalili za mauaji ya kiholela ya wamarekani weusi ambayo yametokea kuwa changamoto kubwa kwa idara ya mahakama nchini na adha ya kibaguzi mwaka hata mwaka.Hali hiyo imesababisha kutokuwepo kwa imani baina ya walinda usalama na jamii wanazohudumia.Gavana wa Minnesota Mark Dayton,amewataka maafisa wa uchunguzi wa jimbo hilo kuchunguza kisa hicho,huku akisema kuwa Castile hangeuliwa angalikuwa mmarekani mweupe.