Rais awaonya wanasiasa

Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa wanasiasa kusalia watulivu na kufanya kampeini zao kwa njia ya amani ili kujenga taifa dhabiti na lenye nguvu. Rais aliwaonya wanasiasa dhidi ya kujihusisha na mizozo ya kisiasa na uchochezi huku akitaja maovu hayo mawili kuwa njia potovu za kutumia kupata uongozi.A� RaisA� Kenyatta alikuwa akiongea alipoweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa hospitali yaA� Dikkir Level 4 katika kaunti yaA� Narok. Akielezea ruwaza yake kwa taifa dhabiti, rais alisema kuwa pindiA� tu ujenzi wa hospitali hiyo utakapokamilika, serikali ya taifa itaweka vifaa maalum vya matibabu kupitia kwa huduma ya mpango wa usimamizi wa vifaa ili kuwawezesha wakazi wa kupata huduma maalum za matibabu katika eneo bunge laA�A� Emurua Dikkir.A� Serikali itatumia zaidi ya shilingi milioni 200 kujenga hospitali hiyo ambayo itakuwa na mashine ya kisiasa ya x-ray, chumba na vifaa vya upasuaji miongoni mwa vifaa vingine vya kisasa vya matibabu na maabara.

Rais alisisitiza kuwa lengo kuu la serikali yakeA� ni kuhakikisha kuwa kuna maendeleo sawa katika maeneo mbalimbali kote nchini kwa minajili ya kuyaendeleza maeneo ambayo awali yalikuwa yametengwa