Rais Apendekeza Wafula Chebukati Kuteuliwa Kama Mwenyekiti Wa IEBC

Rais Uhuru Kenyatta amempendekeza Wafula Chebukati kwa uteuzi katika wadhifa wa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini (IEBC). Pia amewapendekeza Consolata Nkatha Bucha, Boya Molu, Dr Roselyn K. Akombe, balozi Dr. Paul Kurgat, Margaret Wanjala Mwachanya na Profesa Abdi Guliye kwa uteuzi kama makamishna wa tume ya (IEBC). Taarifa kutoka Ikulu imesema kwamba Rais amewasilisha majina yao kwa Bunge ili kuchunguzwa na hatimaye kuidhinishwa kwa mujibu wa katiba.