Rais Aonya Vyuo Vikuu Dhidi Ya Kutoa Vyeti Kwa Njia Ya Ulaghai

Rais Uhuru Kenyatta, ameonya vyuo vikuu dhidi ya utoaji shahada za digrii kwa wanasiasa wanaotafuta kununua hati hizo. Rais alisema kwamba chuo kikuu chochote ambacho kitatoa hati hizo kwa njia ya ulagai kitachukuliwa hatua za kisheria.A� Alikuwa kiongea kwenye chuo kikuu cha Kibabii huko Bungoma alipoongoza hafla ya kwanza ya kufuzu chuoni humo. Aidha, Rais alishauri taasisi za elimu ya juu kujihadhari dhidi ya uwezekano wa kugeuzwa kuwa za kikabila ama kuzushwa kwa hadhi zao na kubakia kuwa chanzo cha ajira. Pia alihimiza vyuo vikuu kutumia fedha zinazopatikana chini ya mipango ya masomo kwaA� wanafunzi wa kujitegemea, kufadhili shughuli nyingi zaidi za utafiti na huduma kwa jamii. Aidha, Rais alisema serikali itaendelea kufadhili vyuo vikuu vya umma lakini taasisi hizo sharti zijitafutie fedha za kufadhili huduma za maktaba na shughuli nyingine za utafiti.