Rais ahimiza viongozi kujiepusha na siasa ambazo zaweza leta machafuko nchini

Rais Uhuru Kenyatta amewahimiza viongozi wa kisiasa wasijihusishe kwenye siasa ambazo zaweza kuitumbukiza nchi hii kwenye machafuko. Akiongea jana alipokuwa mwenyeji wa ujumbe wa zaidi ya watu elfu-15 kutoka kaunti za Kisii na Nyamira katika ikulu ya Nakuru rais alisema hakuna haja ya kuwa na hali ya taharuki hapa nchini kila baada ya miaka mitano kwa sababu ya siasa akisema viongozi wapasa kuzingatia siasa zinazotilia maanani masuala muhimu na wala sio makabila. Kadhalika kiongozi wa nchi alisema kwamba ajenda ya chama cha Jubilee kwa nchi hii inajumuisha uzinduzi miradiA�A�ambayo itabadilisha maisha ya wananchi moja kwa moja. Naibu rais William Ruto aliukashifu upinzani kwa madai ya kuwagawanya Wakenya kwa misingi ya kikabila huku ukipuuza masuala halisi yanaokumba nchi hii. Ruto alisema upinzani wapasa kuzingatia siasa zinazoangazia masuala muhimu. ViongoziA�A�hao wawili waliishukuru jamii ya Abagusii kwa kuwaunga mkono wakati wa uchaguzi mkuu tarehe 8 mwezi Agosti.