Rais ahakikishia wafanyabiashara amani wakati wa marudio ya uchaguzi wa urais

Rais Uhuru Kenyatta amehakikishia jamii ya wafanyibiashara kuwa taifa hili litakuwa na amani wakati na baada ya marudio ya uchaguzi wa urais. Akihutubia wanachama wa chama cha wenye biashara humu nchini katika ikulu ya Nairobi, rais Kenyatta aliwahimiza wawekezaji kuendelea kuwekeza hapa nchini kwani serikali imechukau hatua kuhakikisha biashara zao zimelindwa. Mwenyekiti wa chama cha wafanyibiashara, Karole Kariuki alisema jamii hiyo inajitahidi kuimarisha imani ya wawekezaji kwa taifa hili na akahimiza wanahabari wakiwemo wale wanaotumia mitandao ya kijamii kujiepusha na habari zinazoweza kuibua taharuki humu nchini. Chama hicho kiliwasilisha ripoti kuhusu athari za uchaguzi kwa uchumi wa taifa iliyoonyesha kuwa taifa hili lilipoteza takriban shilingi bilioni 100 kufuatia uamuzi wa mahakama ya juu kuhusiana na uchaguzi wa urais.