Rais Adama Barrow ateuwa tume ya kuchunguza mali za aliyekua rais nchi hiyo

Rais Adama Barrow wa Gambia A�ameteuwa tume ya kuchunguza mali za aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo – Yahya Jammeh. Kiongozi huyo wa zamani anashtumiwa kwa kuiba zaidi ya A�milioni- 50 kutoka kwa serikali kabla ya kuitoroka nchi hiyo mapema mwaka huu. Tume hiyo itachunguza pia kampuni mbali mbali za Umma zinazodaiwa kuhusiana na A�Jammeh. Rais huyo wa zamani ambaye aliitawala Gambia kwa muda wa miaka 22, alikuwa akiendesha biashara mbali mbali, zikiwemo za kuoka mikate na pia mashamba ya kilimo. Awali, Jammeh alikataa matokeo ya uchaguzi wa mwaka uliopita lakini baadaye alisalimu amri baada ya nchi jirani kutisha kuingilia kijeshi mzozo huo.