Raila Odinga atamatisha ziara yake ya mwisho ya kampeini Busia

Mgombeaji urais wa muungano wa (NASA) Raila Odinga alitamatisha ziara yake ya mwisho ya kampeini katika kaunti ya Busia na ahadi za kuwasaidia akina mama na wazee katika jamii.A� Raila alisema kuwa iwapo atachaguliwa tarehe 8 mwezi Agosti akina mama walio na watoto na ambao hawajaolewa watakuwa na fedha za kufanyia biashara huku pesa za wazee zikiongezwa . Pia alisisitiza kuhusu swala la elimu ya msingi na upili bila malipo na kusema kuwa elimu ni haki ya kila mtoto. Odinga pia alizungumzia mipango ya serikali ya kubuni vituo vya kuhifadhia mabohari katika eneo la Naivasha na kuonya kuwa iwapo atachaguliwa , jambo hilo halitatekelezwa .A� Kulingana na Odinga, hatua hii inalenga kulinda kazi za wale wanaotegemea bandari. Alitoa wito kwa wakaazi waA� Busia kujitokeza kwa wingi ili kumpigia kura siku ya Jumanne ili kuhakikisha miradi ya maana inatekelezwa kikamilifu.