ODM kupunguza ada za usajili wa waniaji wa kike na walemavu

Kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga amesema chama hicho kitapunguza ada ya usajili wa wawaniaji wa kike, walemavu na makundi yaliyotengwa. Odinga alisema hatua hiyo inanuia kuwahimiza wanawake wengi zaidi kuwania nyadhifa mbalimbali za uongozi. Odinga alisema chama hicho kinaunga mkono sheria ya usawa wa kijinsia na kitatenda jukumu lake ili kufanikisha utekelezaji wa sheria hiyo. Odinga ambaye anakutana na wawaniaji wanawake katika chuo kikuu cha Multimedia alikariri kuwa chama hicho kitahakikisha uteuzi wa wawaniaji utafanyika kwa njia huru na ya haki. Aidha alisema chama hicho kitagatua bodi yake ya uchaguzi ili kurahisisha utendakazi.