Raila Odinga akutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa rais mstaafu Daniel Arap Moi nyumbani kwake Kabarak

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga jana alikutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa rais wa taifa hili Daniel Arap Moi ,nyumbani kwake Kabarak akiandamana naA� viongoi wengine wa chama cha ODM.Viongozi hao wawili walizungumzia maswala ya umuhimu kwa taifa hili,hasa hali ya kisiasa ilivyo hapa nchini.

 

Kulingana na taarifaA� iliotolewa na chama cha ODM viongozi hao waligusia maswala kadhaa muhimu.Hii ilikuwa mara ya kwanza kwaA� OdingaA� kumtembelea rais mstaafu Moi,ambaye aliliongoza taifa hili kwa muda mrefu.Viongozi kumi wa kisiasa wameunga mkono mkutano baina ya Odinga na rais Kenyatta.Hivi majuzi aliyekuwa gavana wa Kiambu William Kabogo alikutana na Odinga na kuzua hisia tofauti kuhusu mwelekeo wa kisiasa hapa nchini.Mnamo wiki za hivi karibuni Raila amekutana na mabalozi wa kigeni walio humu nchini akiwemo balozi wa Marekani Robert Godec,Nick Hailey wa Uingereza na wafanyabiashara mashuhuri wa Nairobi.