Raila Na Joho Waelekea Ghana Kushuhudia Kuapishwa Kwa Rais Mpya

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliondoka hapa nchini leo asubuhi kuelekea nchini Ghana kuhudhuria kuapishwa kwa rais mteule wa nchi hiyo Nana Akufo-Addo hapo kesho .Odinga anaandamana na naibu kiongozi wa chama cha ODM ,ambaye pia ni gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho. Kwenye kitandazi cha twita ,kiongozi huyo wa upinzani alimpongeza rais wa nchi hiyo anayeondoka John Dramani Mahama, kwa kuzingatia demokrasia na kutoa mwongozo kwa nchi yake ya Ghana na bara la Afrika kwa jumla.A� Addo alimshinda rais Mahama kwa kupata asilimia 53.8 ya kura zilizopigwa dhidi ya asilimia 44.4. Addo alihudumu katika wadhifa wa waziri wa mashauri ya kigeni na mwanasheria mkuu katika serikali ya chama chaA�A� New Patriotic a��NPP,kati ya mwaka 2001 na 2009 na amewahi kuwania urais mara mbili .