Raila adai chanjo dhidi ya pepo punda ilikuwa ya kuwafanya wasichana tasa

Mgombeaji Urais wa muungano wa NASA, Raila Odinga amedai kwamba mpango wa chanjo wa mwaka  2014 dhidi ya ugonjwa wa pepo punda humu nchini ulikuwa hatua ya ki-makusudi ya kuwafanya wasichana kuwa tasa. Raila amesema madai yake ni kutokana na matokeo ya utafiti wa ki-sayansi kutoka taasisi nne zilizobaini kuwa chanjo hiyo haikustahili kutumiwa. Kwa kukubalia na pingamizi za kanisa katoliki kuhusiana na mpango huo wa Chanjo, Raila alisema matokeo ya utafiti wa ki-matibabu yameonyesha kwamba ma-elfu ya wanawake wa umri wa miaka 14 hadi 49 hawataweza kuzaa iwapo kutakosekana taratibu nyingine za ki-matibabu za kubadili uharibifu huo. Mnamo mwaka 2014, serikali kupitia kwa wizara ya afya ilizindua mpango wa chanjo dhidi ya Pepo punde kote nchini  licha ya pingamizi kali kutoka kwa kanisa katoliki. Kanisa hilo lilihoji kwamba  chanjo hiyo ilikuwa mchanganyiko wa dawa  zenye uwezo wa kufanya wanawake kukosa kuzaa. Odinga sasa anataka uchunguzi kamili kufanya ili kukadria uharibifu uliotokana na mpango huo wa chanjo. Wakati huo huo; Odinga ameyataja kuwa yasiyo na msingi madai eti utawala wake utahangaishwa vibaya endapo atashinda katika marudio ya uchaguzi wa Urais.