Raila Azuru Maeneo Ya Magharibi Mwa Kenya

raowestern

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga leo anazuru maeneo ya Shinyalu na Ikolomani huku ziara yake magharibi ya nchi ikingia siku ya pili. Raila atahutubia mikutano ya hadhara katika masoko ya Shanderema, Shinyalu na Khayega. Baadaye ataelekea katika eneo bunge la Ikolomani ambako atahutubia mikutano kadhaa ya hadhara na kuhitimisha siku katika mji wa Shisicheri.

Ziara ya Raila katika kaunti ya Kakamega inalenga kuimarisha udhibiti wa ngome yake ya kisiasa katika eneo hilo ambalo lilimpigia kura kwa wingi katika uchaguzi mkuu wa mwaka-2013. Hapo jana, Raila alitilia shaka utendakazi wa serikali ya Jubilee tangu rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto washike hatamu za uongozi.

Alisema serikali ya Jubilee imeshindwa kutekeleza ahadi ilizotoa kwa wananchi kabla ya uchaguzi mkuu uliopita. Ziara ya Raila yenye kauli mbiu, a�?Matokeo, sio ahadi mpya juu ya ahadi nyingine a�? inalenga kudadisi iwapo serikali ya Jubilee imetekeleza ahadi ilizotoa kabla ya uchaguzi mkuu kwani imezongwa na visa kadhaa vya ufisadi