Raila awataka wachapishaji na waandishi kutoa vitabu zaidi kuhusu maovu ya kijamii

 

Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga amewataka wachapishaji na waandishi kutoa vitabu zaidi kuhusu maovu ya kijamii kama vile ufisadi na ukabila katika hatua ya kuleta ufahamu miongoni mwa wakenya.

Akiongea wakati wa kufunguliwa rasmi kwa maonyesho ya kimataifa ya vitabu ya Nairobi katika kituo cha Sarit center hapa jijinii, Odinga alisema waandishi wanajukumu la kutoa nyenzo kwa nchi hii zinazogusia utajiri wa utamaduni wa wakenya na maadili katika jamii. Aliwahimiza wachapishaji kuwekeza zaidi katika vitabu vya kimtandao na vile vya sauti ili kuwafikia watu zaidi.

Mwenyekiti wa chama cha wachapishaji vitabu nchini Lawrence Njagi alizitaka taasisi za elimu kuimarisha tabia ya usomaji vitabu na kuimarisha uvumbuzi na uangavu ili wanafunzi wapate ujuzi wa kutosha katika ulimwengu unaobadilika kila wakati.

Maonyeshi hayo ya kimataifa ya vitabu yalianza Jumatatu huku zaidi ya waonyeshaji vitabu 70 wa humu nchini na 20 wa kimataifa wakishiriki kwenye tukio hilo.