Raila awashtumu wajumbe wa mataifa ya magharibi kuingilia maswala ya nchi

Kiongozi wa muungano wa NASA, Raila Odinga amewashtumu wajumbe wa mataifa ya magharibi kwa kuingilia maswala ya nchi hii huku wakipuuza kile alichokitaja kuwa dhuluma zinazotelezwa na polisi. Raila aliyasema hayo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha City ambako viongozi wa NASA walikuwa wamekusanyika kufariki familia za waathiriwa wa kile kinachodaiwa kuwa dhuluma za polisi. Haya yamejiri huku kukiwa na ripoti kwamba marekani inamshinikiza kiongozi huyo wa upinzani kusitisha mipango yake ya kujiapisha ikisema ni kinyume cha katiba. A�Kiongozi huyo wa upinzani alitoa wito kwa serikali kufidia familia zilizopoteza wapendwa wao wakati wa maandamano kabla na baada ya marudio ya uchaguzi wa urais tarehe 26 mwezi oktoba. Alidai kuwa serikali imekataa kuwajibikia watu 215 ambao anadai ni waathiriwa wa kile anachokitaja kuwa dhuluma zinazotekelezwa na polisi.