Raila awakashifu wanachama wa chama cha jubilee

Mgombea urais wa muungano wa NASA Raila Odinga amewakashifu wanachama wa chama cha Jubilee kutokana naA� shutuma zao za mara kwa mara kuhusu mikakati yake yaA� kukusanya pesa kwa kampeni zake. Akiongea katika kaunti ya Kajiado, Raila alisema kukusanya fedha kutoka kwa wahisani ni tukio ambalo hujiri kote duniani. Alisema mikakati kama hiyo ni jambo la kawaida kote duniani hata katika demokrasia zilizostawi. Alisema mikakati hiyo ya muungano wa NASA inaongozwa na azma ya watu. Chama cha JubileeA� kimekosoa mpango huo kikisema ni njama ya kuwapunja Wakenya pesa zao walizopata kwa bidii. Rais Uhuru Kenyatta jana alisema kwamba upinzani sasa uko fukara kwani magavana ambao walikuwa wakifadhili shughuli zake wakitumia fedha za kaunti walishindwa kwenye uchaguzi.