Raila atao changamoto kwa serikali za kaunti kuhakikisha ugatuzi unafaulu

Kiongozi wa NASA Raila Odinga ametoa changamoto kwa serikali za kaunti kuweka mikakati kuhakikisha kuwa ugatuzi unafaulu .Akihutubu jana kwenye bunge la kaunti ya Kisumu,Raila alitoa wito kwa serikali na bunge la kaunti hiyo kushirikiana ili kutoa huduma bora kwa wakazi. Aliwataka kuepuka kulumbana kuhusu maswala duni na badala yake kuelekeza juhudi zao katika kuwahudumia wakazi . Wakati huo huo , Odinga ameitaka serikali kukoma kuwatisha na kuwahadaa wafwasi wa NASA .Aliwakashifu polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi kuwatawanya waandamanaji,huku akielezea masikitiko yake kuhusiana na vifo ambavyo vimetokea kufwatia maandamano.