Raila asisitiza kuwa wako tayari kwa uchaguzi mpya iwapo tume ya IEBC itafanyiwa marekebisho

Mwaniaji urais wa Muungano waA� National Super Alliance almaarufu NASA Raila Odinga amesisitiza kuwa wako tayari kwa uchaguzi mpya wa urais iwapo tume huru ya uchaguzi na mipaka a��IEBC itafanyiwa marekebisho yanayohitajika. Raila alisema kuwa marekebisho muhimu katika tume hiyo yatatoa fursa sawa kwa wawaniaji wote na kuimarisha demokrasia na ustawi nchini. Kinara huyo wa muungano wa NASA alisema kuwa inashangaza kuwa kampuni ya Safaricom inakanusha kuhusishwa na hitilafu zilizokumbaA� uchaguzi uliopita huku akishangaa namna takwimu zingetumwa katika maeneo mengine bila kutumia mitandao ya kampuni hiyo. Alitaja kisa huko Narok ambapo kituo cha kupiga kura kilichokuwa na wapiga kura 500 waliosajiliwa kiliishia kutoa kura elfu tano kwa rais. Raila alikuwa akiongea katika makao makuu yaA� Okoa Kenya baada ya kukutana na viongozi wa jamii ya Maasai kutoka maeneo ya Kajiado, Narok, Laikipia, Samburu na Marsabit ambapo alisema kuwa uungwaji mkono wao ulikuwa imara katika muungano huo waA� NASA.