Raila asimamisha maandamano kwa heshima ya waliokufa

Kiongozi wa upinzani Raila OdingaA� ametangaza kusimamishwa kwa muda kwa maandamano dhidi ya tume ya uchaguzi a��IEBC, kwa heshima ya wafwasi na familia ambazo zimepoteza wapendwa wao, wanaodaiwa kupigwa risasi na polisi. Kwenye taarifa, kiongozi huyo wa upinzani aliwashauri wafwasi wa NASA kusitisha maandamano kwa sasa,akisema atatoa mwelekeo wakati wa maadhimisho ya siku ya mashujaa. Odinga amesema NASA inasikitishwa sana na mauaji na ukatili unaodaiwa kutekelezwa na polisi,hasa katika maeneo yanayoaminika kuwa ngome ya upinzani .Kiongozi huyo upinzani kadhalika amedokeza kuwa wanatafakari hatua za kuchukua dhidi ya inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinet na kaimu waziri wa usalama wa taifa Dr. Fred Matianga��I kuhusiana na vitendo hivyo.Mapema Mahakama kuu ilisitisha kwa muda utekelezaji wa agizo la serikali la kupiga marufuku maandamano ya mrengo wa NASA katika maeneo ya kati kati ya miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.