Raila arejea nchini kutoka Zanzibar

Kiongozi wa NASA Raila Odinga alirejea humu nchini jana jioni baada ya ziara yake ya siku nne huko Zanzibar. Mnamo siku ya ijuma iliyopita ghasia zilizuka wakati kiongozi huyo wa upinzani alipowasili A�kutoka ziara ya siku 10 nchini Marekani . Raila amerejea nchini siku 2 tu baada ya mahakama ya juu katika kaunti ya Kitui kusitisha kwa muda hoja ya kujadili na kuasisi bunge la wananchi katika kaunti 47. Kulingana na Raila,bunge hilo la mwananchi linalojumuisha viongozi waliochaguliwa,makundi ya kijamii,viongozi wa dini na wananchi wa kawaida linawapa wakenya fursa ya kujiamulia mustakabali wao moja kwa moja kwa mujibu wa katiba. A�Kufikia sasa kaunti 12 kati ya kaunti 19 zinazoegemea mrengo wa NASA A�tayari zimepitisha hoja.