Raila apinga matokea ya mapema ya urais

Kiongozi wa muungano wa NASA Raila Odinga leo asubuhi alitoa taarifa ambapo alilalamikia matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yakiwasilishwa moja kwa moja kwenye mtandao wa IEBC na akaitaka tume hiyo kukagua fomu nambari 34A. Raila alisema matokeo hayo yaliyokuwa yakiwasilishwa si halali akidai kuwa tume hiyo haikukagua fomu nambari 34A mbele ya maajenti wa NASA kabla ya kutoa matokeo hayo. Hata hivyo IEBC inasisitiza kwamba upeperushaji matokeo hayo huenda ukasababisha hali ya wasi wasi humu nchini. Katika taarifa chama cha, Jubilee kupitia katibu mkuu wake Raphael Tuju kilikanusha madai hayo kikisema IEBC inazingatia sheria.