Raila akariri hatashiriki kwenye uchaguzi iwapo matakwa yao hayatashughulikiwa

Mgombea urais wa muungano wa NasaA� Raila Odinga amekariri kuwa hatashiriki kwenye uchaguzi wa urais wa tarehe 17 mwezi ujao,iwapo matakwa ya muungano huo kwa tume ya IEBC hayatashughulikiwa. Akiongea kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kamukunji mtaa wa Kibra, Odinga alisema kuwa upinzani haukufurahia habari walizopata kutoka tume ya uchaguzi kwamba kampuni ya uchapishaji ya AlghurairA� tayari imepewa kandarasi ya kuchapisha karatasi za uchaguzi mpya wa urais licha ya pingamizi zao. Odinga pia alidai tume ya uchaguzi imedinda kushughulikia malalamishi yao ikiwemo kutimuliwa kwa maafisa wote waliohusishwa na dosari zilizoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu wa tarehe nane mwezi jana. Alionya kuwa iwapo tume ya IEBC haitazingatia malalamishi yao, Nasa huenda ikazindua harakati za kuwatimua makamishna wa IEBC.