Raila aikashifu serikali kwa kutoshughulikia ufisadi

Kiongozi wa muungano wa Cord, Raila Odinga kwa mara nyingine ameikashifu serikali kwa kutoshughulikia swala la ufisadi hapa nchini. Akiongea wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku tatu katika kaunti ya A�Turkana, Raila alitoa mfano wa kashfa inayoghubika shirika la huduma za vijana kwa taifaA� NYS, akisema ni sifa mbaya kwa serikali. Alitoa wito kwa wakazi wa kaunti ya Turkana kujitokeza kwa wingi kupigia kura muungano wa upinzani wa NASA wakati wa uchaguzi mkuu ujao. Raila pia alitumia fursa hiyo kuishutumu serikali kwa kile alichokitaja kuwa kujikokota katika kutatua mgomo wa madaktari akidai kwamba matakwa yao yanaweza kutimizwa. A�Mwenyeji wake gavana Josphat Nanok alielezea imani yake kwamba muungano wa NASA utapata idadi kubwa ya kura katika uchaguzi mkuu ujao. A�