Raila adai walinzi wa maafisa wa IEBC wameondolewa

Kinara wa muungano wa NASA Raila Odinga amedai kuwa walinzi wa baadhi ya maafisa wa tume ya IEBC wameondolewa. Raila anadai pia maafisa hao wamekuwa wakipokea vitisho kabla yaA� kuandaliwa kwa marudio ya uchaguzi wa urais wa tarehe 17 mwezi ujao, akitaja hali hiyo kuwa isiyofaa. Akiwahutubia wanahabari katika makao makuu ya Nasa kabla ya kupeleka kampeini zake huko Machakos, Raila aliongeza kuwa muungano wa Nasa utahudhuria mkutano uliopendekezwa wa wadau na tume ya IEBC lakini akahofia kuwa tume hiyo huenda isiweze kushugulikia ipasavyo malalamishi yake kulingana naA� hali ilivyo sasa. Wakati huo huo ,muungano wa NASA umezindua akaunti ya kupokeaA� michango ya kampeini kutoka kwa wafuasi wake.