Raila aahidi wakenya serikali bora akichaguliwa

Mgombea urais wa muungano wa-NASA Raila Odinga, anawaahidi wakenya kwamba serikali yake itabuni mazingira bora ili biashara ziweze kunawiri akichaguliwa kuwa rais tarehe 8 mwezi Agosti. Akiongea huko Bomet alipoendeleza kampeni zake, kiongozi huyo wa upinzani alisema kampuni nyingi zinafungwa ama kupunguza wafanyikazi hivyo basi kuongeza kiwango cha ukosefu ajira hapa nchini.

Wakati huo huo, Raila aliushtumu uongozi wa Jubilee kwa kuharakisha miradi kadhaa kujaribu kutafuta uungwaji mkono wakati wa uchaguzi mkuu ujao, baada ya kushindwa kutimiza ahadi zake kwa Wakenya. Raila aliwaahidi wakazi kwamba hawatajuta kuuchagua uongozi wa NASA.