Raia wa Tanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini hawalengwi

Raia wa Tanzania wanaoishi nchini Afrika kusiniA� hawalengwi, kwa mujibu wa taarifa rasmi ya wizara ya mashauri ya kigeni ya Tanzania,kufwatia kifo cha mwanafunzi wa uzamifu mjini Johanesburg nchini Afrika Kusini.Adolf Mkenda alisema kuwa mwanafunzi huyo LeonardA� Nafari alifariki dunia baada ya kugongwa na gari karibu na mabweni ya wanafunzi mtani Sofiatown siku 10 zilizopita.Kulingana naA� katibu wa kudumu katika wizara hiyo Adolf Mkenda,wanafunzi na raia wa Tanzania walio nchini Afrika kusini hawana haja ya kuhofia lolote,jinsi inadaiwa.Kifo cha mwanafunzi huyo kimezua hali ya taharuki kwamba wageni nchini humo wanachukiwa na wanalengwa na wenyeji,jinsi ilivyotokea miaka kadhaa ya nyuma.Inadaiwa kuwa kifo hicho kilitokana na dereva wa teksi ambaye hakusimama baada ya kumgonga mwanafunzi huyo tarehe 3 mwezi februari.Wanafunzi wenzake wanadai kuwa waliona kwenye mtandao habari kwamba mwanafunzi huyo alikuwa akilitoroka gari hilo,kabla kugongwa.