Raia wa Nigeria wanaoishi Afrika Kusini waelezea wasiwasi kuhusu ghasia dhidi ya wahamiaji

Raia wa Nigeria wanaoishi nchini Afrika kusini wameelezea wasiwasi kuhusu kuzuka upya kwa ghasia dhidi ya wahamiaji nchini humo huku wakitoa wito kwa maafisa husika kuingilia kati kabla ya hali kuwa mbaya. A�A�Afisi ya rais nchini Nigeria siku ya jumatatu ilitoa wito kwa serikali ya Afrika kusini kuingilia kati na kudhibiti mashambulizi hayo dhidi ya raia wa Nigeria hasa mjini Pretoria. Chama cha raia wa Nigeria nchini Afrika kusini kilidhibitisha kuwa nyumba na biashara za raia wa Nigeria ilivamiwa magharibi ya mji wa Pretoria West. Chama hicho pia kilisema kuwa baadhi ya wanachama wake wamepokea vitisho kupitia kwa simu za rununu. Alitoa wito wa mamlaka husika kulinda nyumba na mali zao. Polisi nchini Afrika kusini wamedhibitisha kuwa maduka yapatayo 20 ambayo huenda yanamilikiwa na raia wa kigeni yaliporwa jijini A�Pretoria usiku.