Raia Nusu Milioni Nchini Guinea Wahudhuria Mkutano Wa Upinzani Mjini Conakary

guinea
Raia nusu milioni nchini Guinea wamehudhuria mkutano wa upinzani mjini Conakary kuibeza serikali ya rais Alpha Conde kutokana na mgogoro wa kiuchumi na visa vya ufisadi. Kiongozi wa chama cha upinzani cha Union of Democratic Forces of Guinea, Cellou Dalein Diallo alisema watu elf-700 walishiriki kwenye maandamano ya kuelekea katika uwanja mmoja mjini Conakry.

Hata hivyo duru nyingine zilisema kuwa watu nusu milioni walihudhuria mkutano huo kama ishara ya kudhihirisha kuchukizwa kwao na utawala wa kiimla wa rais Conde. Diallo alikashfu serikali kwa kusambaratisha mradi wa ufuaji vyuma wa Simandou uliokuwa ukisimamiwa na kampuni moja ya Uingereza kwa jina Rio Tinto, hatua iliyosababisha raia wa Guinea kupoteza ajira.