Raia 43 wahukumiwa vifingo vya maisha gerezani, Misri

Raia 43 wa Misri wamehukumiwa vifungo vya maisha gerezani, huku wengine mamia wakihukumiwaA� vifungo virefu kwa kuhusika katika vurugu wakatiA� rais Mohamed Mursi aliponga��olewa mamlakaniA� na jeshi la nchi hiyo mnamo mwaka wa 2013. Zaidi ya wahalifuA�A� 500 walihukumiwa vifungo vya kati ya miaka 5 hadi 15. Hata hivyo 54 kati yao waliachiliwa huru, akiwemo raia mmoja mwenye uraia wa Ireland Ibrahim Halawa. Halawa alikuwa na umri wa miaka 17 alipotiwa nguvuni na aliteswa sana kwa kipindi cha miaka minne alipokuwa gerezani. Raia mwingine Ahmed Atiwy alikuwa miongoni mwa wale waliotumikia vifungo vya miaka mitano gerezani. Hukumu hiyo ya jumla ilifanywa kwenye gereza la Wadi al-Natroun kaskazini ya mji wa Cairo, kwa mujibu wa shirika moja la kimataifa la kutetea haki za binadamu.