Rafael Nadal ashinda kesi ya madawa ya kusisimua misuli

Mahakama moja jijini Paris imemuamrisha aliyekuwa waziri wa michezo nchini Ufaransa Roselyne Bachelot kumlipa nyota wa tenisi Rafael Nadal dola elfu 14 kwa kudai kuwa mchezaji huyo anatumia dawa haramu michezoni. Nadal alimshtaki Bachelot kwa matamshi yake akisema yalishusha hadhi yake. Mchezaji huyo anayeorodheshwa wa kwanza duniani alitaka kulipwa Yuro elfu mia moja kufidia gharama hiyo baada ya Bachelot kutoa matamshi hayo ya matusi wakati wa mahojiano katika runinga moja. Jaji huyo pia alimtoza Bachelot faini zaidi ya Yuro mia tano kwa matusi.